Ligi Kuu ya Tanzania Bara imesimama kupisha michezo ya kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON 2021 ambapo Tanzania inakabiliwa na michezo miwili katika kipindi cha siku nane
Ijumaa ya wiki hii, Novemba 15 Stars itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Equatoria Guinea katika mchezo wa kwanza wa kundi J ambao utapigwa saa moja jioni
Baada ya mchezo huo, Stars itaelekea nchini Algeria ambako Novemba 19 itaumana na Libya
Stars iko kundi J pamoja na timu za Libya, Equatoria Guinea na Tunisia
Jana kikosi cha kocha Etienne Ndayiragije kilianza mazoezi yanayofanyika dimba la Taifa kuelekea mchezo huo wa nyumbani
Baada ya kushiriki michuano ya Afcon kwa mara ya pili mwaka huu, Stars inawania moja ya nafasi mbili
ADVERTISE HERE