Uongozi wa Yanga umemkabidhi rasmi barua ya kuvunja mkataba aliyekuwa kocha wake Mwinyi Zahera ambaye amerejea kwao kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa
Baada ya Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla kutangaza uamuzi wa kuvunja mkataba wake mapema wiki hii, Zahera kupitia vyombo mbalimbali vya habari alitoa malalamiko mengi likiwemo la kutopewa barua rasmi ya kutimuliwa
Inaelezwa uongozi wa Yanga umemlipa kocha huyo mishahara ya miezi minne (Miwili ya kuvunja mkataba, miwili ya madai) ikiwa ni matakwa ya makubaliano ya kisheria
Zahera alikuwa akipokea kitita cha Tsh Milioni 15 kwa mwezi
Aidha uongozi wa Yanga umeahidi kulipa madai yake mengine kulingana na makubaliano yaliyopo
Zahera amedai kutumia zaidi ya milioni 100 kuihudumia Yanga kwa nyakati tofauti
Mwandila mkataba ulikuwa ukiongoni
Kwa upande wa aliyekuwa kocha Msaidizi Noel Mwandili, yeye ataambulia malipo ya mwezi mmoja tu kwani mkataba wake ulikuwa mbioni kumalizika
Mkataba wa Mwandila ungemalizika Disemba 05 2019