Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewapa wachezaji mapumziko ya siku tano baada ya mchezo dhidi ya Ndanda Fc ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 juzi
Uongozi wa Yanga umesema Mkwasa atatumia muda huo kuandaa program ya mazoezi ya kikosi chake
Mchezo unaofuata wa Yanga ni dhidi ya KMC, utapigwa Novemba 20 kwenye uwanja wa Uhuru
Aidha, Ofisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema timu itafanya ziara ya siku mbili mkoani Mtwara kabla ya kurejea jijini Dar es salaam
ADVERTISE HERE