Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya Ndanda Fc ni mwanzo tu kwani wamejipanga kushinda kila mchezo kwenye ligi
Akizungumza jana baada ya mchezo huo uliofanyika mkoani Mtwara, Tshishimbi alisema baada ya kukosa nafasi ya kucheza makundi kombe la Shirikisho, watahakikisha wanatwaa ubingwa ili msimu ujao warejee kwenye michuano ya Kimataifa
"Baada ya kutolewa kombe la Shirikisho, wachezaji wote tulizungumza na kuweka ahadi lazima tushinde kila mchezo tukianza na huu wa Ndanda," alisema
"Tumejipanga vizuri, tutafanya mambo makubwa ambayo wengi watashangaa"
"Muhimu tunawaomba mashabiki waendelee kutuunga mkono. Tumeanza kufanya kazi na Mwalimu mpya, tutahakikisha tunayaelewa maelekezo yake ili tuweze kufanya vizuri"
Tshishimbi ameendelea na majukumu ya unahodha wa Yanga licha ya mabadiliko ya benchi la ufundi yaliyofanywa na uongozi wa Yanga
Aliteuliwa na Zahera mwanzoni mwa msimu huku Juma Abdul akiachiwa majukumu ya unahodha msaidizi