Pamoja na changamoto ya uwanja, wachezaji wa Yanga leo walionyesha kitu tofauti mkoani Mtwara katika mchezo dhidi ya Ndanda Fc walioibuka na ushindi wa bao 1-0
Wamejitahidi kuweka mpira chini na kupiga pasi nyingi, wakiachana kabisa na ule utaratibu wa kupiga mipira mirefu uliokuwa ukitumika zaidi wakati wa Zahera
Kwa kiasi flani, leo ubunifu wa akina Mapinduzi Balama umeonekana
Enzi ya Zahera, mechi zilizopigwa kwenye viwanja 'vikorofi' kama hapo Nangwanda, walinzi ndio walikuwa wachezeshaji wa timu kupitia mipira mirefu
Yanga hii ya Mkwasa itakuwa tofauti zaidi itakapocheza uwanja wa Uhuru au Taifa
Leo ilianza mchezo taratibu lakini katika kipindi cha pili wachezaji waliongeza kasi kusaka ushindi
Kwa wastani, Mkwasa ameanza vyema japo hakuwa na muda mrefu wa kuiandaa timu
Bila shaka atakitumia kipindi cha mapumziko ya mechi za Kimataifa kuendelea kuingiza mbinu zake kwa wachezaji