Mabadiliko yaharakishwe Yanga

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
7 Nov 2019
Mabadiliko yaharakishwe Yanga

Wakati wanaingia madarakani mwezi May, Wanachama na Mashabiki wa Yanga walikuwa na matumaini makubwa kwa viongozi mpya wakiamini kuwa hatimaye timu imewekwa kwenye mikono salama na sasa mambo yataanza kwenda sawa

Lakini wengi wamepata mshtuko jana baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kubainisha mambo mengi ya ndani ya uongozi yanayoashiria bado kuna mambo hayako sawa

Moja ya ahadi ambazo Dk Msolla alitoa wakati akiingia madarakani ni kusimamia mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uwendeshaji

Nadhani mpaka sasa wengi watakubali huu mfumo wa kutegemea wanachama na mashabiki kuchangia uendeshaji wa timu umeshindwa, ni wakati wa kwenda kwenye mfumo wa kibiashara zaidi ambao ni wa hisa

Pamoja na kampeni kubwa iliyofanyika ambayo iliingiza Milioni 920, lakini kama timu inazuiliwa Hotelini kwa kushindwa kulipia bili ya vinywaji ambayo ni laki tano, hiyo sio dalili nzuri

Hali haijulikani huko kwingine kama kwenye mishahara ya wachezaji na mengineyo ingawa inafahamika mpaka sasa bado iko changamoto kwenye kulipa madeni

Ni wakati kwa Wanayanga kukubali kuwa njia pekee ambayo itaiondoa timu kwenye changamoto za kiuchumi ni uendeshaji wa kisasa

Wanachama wanapaswa kuhoji kuhusu mwenendo wa mchakato wa mabadiliko ulipofikia na sio kuwaachia viongozi pekee waamue huko maofisini

Suala la mabadiliko katika vilabu vyetu hivi linakuwa gumu kwa sababu linagusa maslahi ya baadhi ya watu

Watu hao wako tayari kufanya lolote ili mradi tu kuendelea na mfumo ambao utaendelea kuwanufaisha

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’