Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema yuko mbioni kuanzisha shule ya kulelea vipaji 'Academy' hapa Tanzania
Akihojiwa kwenye kipindi cha SportsXtra cha Clouds FM jana, Mcongomani huyo alisema amevutiwa na mazingira ya hapa Tanzania hivyo pamoja na biashara zake nyingi kuwa nchini Congo, yeye atarejea kuishi hapa
"Natarajia kurejea Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa kujiandaa na Afcon dhidi ya Gabon, baada ya mechi nitarudi tena hapa Tanzania. Mimi napenda sana mnavyoishi hapa, nitawekeza hapa nchini nataka kufungua Academy ya mpira wa miguu"
Zahera alifafanua shule hiyo hiyo itasajili watoto wenye umri kati ya miaka 12 na 16
ADVERTISE HERE