Ligi Kuu ya Vodacom imeingia raundi ya 11 leo kwa mechi sita kupigwa katika viwanja mbalimbali
Singida United inazidi kujichimbia kaburi la kushuka daraja baada ya leo kufumuliwa mabao 5-1 na Lipuli Fc
Singida United ndio timu pekee ambayo bado haijapata ushindi wowote msimu huu ikishika nafasi ya mwisho ikiwa na alama nne kutoka michezo 11
Dk Mwigulu Nchemba, Rais wa timu hiyo ana kazi ya kufanya kuinusuru kuteremka daraja kwani dalili zote zinaonyesha huenda msimu ujao wakacheza ligi daraja la kwanza

Michezo mingine itapigwa kesho Alhamisi, wakati kikosi cha Yanga kitashuka dimbani keshokutwa Ijumaa kuikabili Ndanda Fc kwenye mchezo ambao utapigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara
ADVERTISE HERE