Mchakamchaka wa kusaka tiketi ya kushiriki fainali za michuano ya Afcon 2021, utaanza wiki ijayo ambapo Tanzania itaanza kampeni ya kushiriki michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo kwa kuumana na Equatorial Guinea
Mchezo huo utapigwa Ijumaa 15 Novemba 2019, saa moja usiku kwenye uwanja wa Taifa
Viingilio vya mchezo huo VIP B na C ni Tsh 5,000/- wakati mzunguuko ni Tsh 3,000/-

Kocha Mkuu wa Stars Etienne Ndayiragije anatarajiwa kuweka hadharani kikosi chake leo
Baada ya mchezo huo, Stars itaelekea nchini Libya ambapo Novemba 19 itacheza mechi yake ya pili huko
ADVERTISE HERE