Ukarabati wa Kaunda washika kasi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Oct 2017
Ukarabati wa Kaunda washika kasi
Ukarabati wa uwanja wa Yanga, Kaunda unaendelea ambapo sasa zoezi la kumwaga vifusi vya mchanga linaendelea.

Wakandarasi wanaokarabati uwanja huo wameihakikishia Yanga kuwa hadi kufika mwanzoni mwa mwaka 2018 ukarabati utakuwa umekamilika na uwanja utakuwa tayari kutumika.



Uwanja huo ukikamilika utaiwezesha Yanga kuondokana na gharama za viwanja vya kukodi kwa ajili ya mazoezi.

Aidha uwanja wa Kaunda kitakuwa chanzo cha mapato ya klabu ambapo mashabiki wataweza kuichangia klabu yao kwa kulipa viingilio kushuhudia mazoezi ya Yanga.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema pia klabu yake inakusudia kuutumia uwanja huo katika michezo yake ya nyumbani katika ligi kuu ya Vodacom.

"Tuna eneo takriban ekari 9 tuna kiwanja kikubwa cha kuweza kubeba watu Kama elfu 15 hadi 20, tutaweka proposal na kuweka wazi kwa wadau mbalimbali ambao watakuwa tayari kufanya kazi na sisi na kutuwezesha kujenga uwanja ambao tunaweza kuutumia kwa mechi za Ligi Kama uwanja wetu wa nyumbani, uwanja wa timu za watoto na pia eneo la biashara kwa ajili ya uwekezaji utakaosaidia Klabu kuongeza mapato yake "
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’