Mwinyi Zahera leo aliamua kumwaga mboga! Ni baada ya uongozi wa Yanga kuvunja mkataba wake pamoja na benchi zima la ufundi
Ametaja sababu ambayo anadhani imepelekea yeye kuondolewa Yanga
Amesema uongozi wa Yanga ulimpendekeza kocha Charles Boniface Mkwasa kuwa kocha msaidizi, hakukubaliana na uamuzi huo
"Kwangu mie kitu ambayo inanitoa Yanga ni kukataa kuletewa kocha Msaidizi ambaye ni Charles Mkwasa"
"Sababu nilisimulia nae (Mwenyekiti) mambo mengi na mwenyewe akasema mechi nne haziwezi kutumika kunifukuza mimi, inafaa iwe angalau mechi 10," alisema
Kwa sasa Mkwasa ameteuliwa kuwa Kaimu Kocha Mkuu wakati uongozi wa Yanga ukiendelea na mchakato wa kusaka kocha mpya ambapo Mwenyekiti wa Yanga Dk Msolla amesema mchakato huo unaweza kuwa umekamilika baada ya wiki mbili