Balinya 'afurahi ki-aina' Zahera kuondolewa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Nov 2019
Balinya 'afurahi ki-aina' Zahera kuondolewa Yanga

Mmoja wa wachezaji ambao watakuwa na furaha baada ya kocha Mwinyi Zahera kuondoshwa Yanga, ni Juma Balinya

Chini ya Zahera Balinya alikuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza pamoja na kuanza vyema wakati wa maandalizi ya msimu timu ilipokuwa chini ya Noel Mwandila mkoani Morogoro

Kwa nyakati tofauti Balinya alibainisha waziwazi kuwa Zahera alikuwa 'akimbania'

Chapisho aliloweka Balinya kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya Zahera kuondolewa Yanga

Wakati akiwa Polisi Fc ya Uganda msimu uliopita ambao aliibuka kuwa mfungaji bora wa ligi ya nchi hiyo, Balinya alikuwa akicheza namba tisa au kumi

Lakini mechi za karibuni, Zahera alimpa dakika chache huku akimtumia kama winga isipokuwa mchezo wa juzi dhidi ya Pyramids Fc

Inaelezwa uamuzi wa kumuondoa Zahera ulikuwa hauepukiki kwani sio Balinya tu, baadhi ya wachezaji hasa wapya walishindwa kuelewa mbinu zake

Balinya hatalisahau tukio lililomtokea mkoani Mwanza pale alipoachwa nje kwenye kikosi kilichopaswa kuikabili Pyramids Fc

Mshambuliaji huyo aliongezwa kikosini baada ya kelele za mashabiki na baadhi ya viongozi kuhoji kwa nini yuko nje wakati timu ina wachezaji pungufu

Anaanza maisha mapya chini ya kocha mpya, pengine mambo yatamnyookea sasa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
8h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’