Katika kuhakikisha timu inarejea haraka kwenye ushindani, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano Hussein Nyika anarejeshwa katika Kamati ya Mashindano
Mapema leo, Kamati ya Utendaji ya Yanga ililivunja benchi la Ufundi pamoja na Kamati ya Mashindano kwa lengo la kusukwa upya
Nyika amekuwa kiongozi wa Yanga kwa muda mrefu akihusika zaidi na kamati hizo mbili
Ni mmoja wa viongozi wa awamu iliyopita ambao walijiuzulu nafasi zao ili kupisha uchaguzi ambao uliwaweka madarakani Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla na timu yake
Msimu uliopita Nyika alitupiwa sana lawama akidaiwa kukwamisha usajili wa baadhi ya wachezaji
Hata hivyo hivi karibuni mwenyewe amefichua kuwa Yanga haikuwa na fedha, usajili waliofanya msimu uliopita, kwa kiasi kikubwa ulitokana na michango waliyokuwa wakichangishana