Uongozi wa klabu ya Yanga umechukua uamuzi sahihi kuikabidhi timu kwa kocha Charles Mkwasa kipindi hiki cha mpito
Mkwasa amekuwa sehemu ya Yanga tangu msimu ulipoanza akiwa Katibu wa Kamati Ufundi
Hakuna shaka tutashuhudia mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake
Pengine ule utamaduni wa Yanga kushambulia kupitia mawinga ataurejesha rasmi
Aidha uzoefu wake kwa soka la ndani, itakuwa chachu kwa Yanga kufanya vizuri
Ujio wa kocha mpya pia utatoa nafasi kwa baadhi ya wachezaji ambao walikuwa hawapewi nafasi na kocha aliyepita kuonyesha uwezo wao
Suala la baadhi ya wachezaji kutumika katika nafasi zisizo sahihi litakuwa limemalizika rasmi
Muhimu ni kwa mashabiki kuendelea kuiunga mkono timu yao na zaidi wasimuweke kocha katika presha mapema
Pengine nae anaweza akahitaji mechi kadhaa kuweza kutengeneza kikosi chake