Ngoma aikana Polokwane asaini miaka miwili, Tambwe nae tayari

Admin By Admin
β€’
27 Jun 2017
Ngoma aikana Polokwane asaini miaka miwili, Tambwe nae tayari
Mshambuliaji wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, Donald Ngoma anayewindwa na Wekundu wa Msimbazi , amesaini miaka miwili kuendelea kuitumikia Yanga.

Mapema jana, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwassa alisema Ngoma yuko kwenye mipango ya kocha George Lwandamina na tayari uongozi wa timu hiyo ulikuwa umemalizana nae kuhusu kuongeza mkataba mpya na alitarajiwa kusaini leo.

Kuna taarifa kuwa viongozi wa klabu ya Simba nao walizungumza nae.

Aidha Yanga imemalizana na mshambuliaji wake Amissi Tambwe ambaye tayari amerejea jijini Dar es salaam kutoka Burundi alikokuwa mapumziko.

Mkwassa pia amesema Yanga itaachana na mlinzi wake wa kati Vicent Bossou raia wa Togo ambaye mkataba wake umemalizika na wameshindwa kufikia nae makubaliano ya mkataba mpya.

Aidha, Yanga imesajili wachezaji watatu wa kigeni ambapo Mkwassa amesema uongozi utawatambulisha wachezaji hao kwa utaratibu maalum muda utakapofika.

Wachezaji hao watatu wanategemewa kuziba nafasi za Vicent ossou, Haruna Niyonzima na Justine Zulu ambaye huenda akaachwa baada ya kushindwa kuonyesha makali yake Jangwani.

Hi ni habari njema kwa mashabiki wa Yanga baada ya klabu kufanikiwa kuwabakisha wachezaji hao muhimu. Yanga bado itaendelea kuwa imara msimu ujao.

Mkwassa ambaye amegoma kuweka hadharani majina ya wachezaji watatu wa kigeni mpaka watakapotambulishwa, amesema wana viwango zaidi ya hao walioondoka.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’