Yanga imefungwa na timu bora, tujipange mwakani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Nov 2019
Yanga imefungwa na timu bora, tujipange mwakani

Kwa Mwanayanga aliyepata nafasi kutazama mchezo wa marudiano kati ya Pyramids Fc dhidi ya Yanga uliopigwa nchini Misri, atakubali kuwa Pyramids Fc ilikuwa bora zaidi ya Yanga kwa uwezo wa kitimu na hata mchezaji mmoja mmoja

Ni timu ambayo inasadifu uwekezaji mkubwa ambao matajiri wa timu hiyo wamefanya

Pyramids Fc nadhani hawana muda mrefu wataanza kupata mafanikio makubwa katika soka la Afrika

Kwa Yanga yetu, nadhani bado kuna kazi kubwa inapaswa kufanyika

Pengine viongozi ni vyema wakatumia ushiriki huu wa mwaka huu kama somo ili kama timu itapata nafasi ya kushiriki msimu ujao, wafahamu nini wanapaswa kufanya ili timu iweze kufanya vizuri

Kwa timu ilipofikia wachezaji wanastahili pongezi, wamejitumia kwelikweli. Sidhani kama yupo wa kulaumiwa kwa upande wa wachezaji kwani juhudi zao zimeonekana kwenye michuano hii

Wakati mwingine unaweza kuelewa kwa nini Zahera alichukizwa na lawama alizokuwa anapewa baada ya timu kufungwa kwenye mchezo wa kwanza jijini Mwanza

Ni kwa kuwa alifahamu uwezo wa timu yake kulinganisha na Pyramids Fc

Ingawa kimsingi hawezi kukwepa lawama moja kwa moja kwa kuwa ni yeye aliyependekeza usajili wa wachezaji wote, japo kwa upande mwingine nae anajitetea kuwa usajili aliofanya ulikuwa kwa ajili ya Ligi

Kwa maana wakati wanasajili Yanga haikuwa na taarifa ya kushiriki michuano ya Kimataifa ambapo taarifa waliipata wakati michakato yote ikiwa imekamilika

Timu inahitaji maboresho

Safu ya ushambuliaji bado ni changamoto. Uongozi wa Yanga hauwezi kukwepa kuongeza nguvu wakati wa usajili wa dirisha dogo

Timu inahitaji washambuliaji wenye uwezo kuwazidi waliopo

Changamoto ya mabao bado itaendelea kuisumbua Yanga hata kwenye ligi kutokana na aina ya washambuliaji waliopo

Habari njema ni kuwa dirisha dogo la usajili litafunguliwa wiki chache zijazo hivyo Yanga itakuwa na nafasi ya kujiimarisha kabla ligi haijachanganya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’