Mchezo wa pili wa kombe la Shirikisho kati ya Pyramids dhidi ya Yanga umemalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 3-0
Pyramids wametinga makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1 wakiwa pia wameshinda mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Mwanza kwa mabao 2-1
Ulikuwa ni mchezo ambao wachezaji wa Yanga walituma sana lakini ubora wa Pyramids ulikuwa chachu kwao kupata ushindi mwingine nyumbani
Aidha Yanga ilikabiliwa na changamoto ya majeruhi baada ya Ally Ally na Lamine Moro wote kuumia
Moro aliumia wakati Yanga ikiwa tayari imeshatumia nafasi zake zote tatu za mabadiliko hivyo kulazimika kucheza na wachezaji 10
Nahodha Papy Tshishimbi alilazimika kurudi nyuma kucheza namba tano sambamba na Ally Mtoni
Pyramids walifunga bao la tatu wakati wa muda wa majeruhi baada ya timu hiyo kufanya shambulizi la kushitukiza
Yanga imemaliza rasmi kampeni yake ya michuano ya Kimataifa na sasa inarejea kwenye mikikimikiki ya ligi kuu