Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi kuelekea mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids FC ambao utapigwa baadae leo
Dk Msolla amesema timu imeandaliwa vizuri na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo utakaopigwa saa tatu usiku
Dk Msolla amesema viongozi waliosafiri na timu Misri, benchi la ufundi pamoja na wachezaji, wameahidi kupambana ili kuibuka na ushindi
"Tumeshazungumza na wachezaji pamoja na viongozi waliotangulia Misri wametuhakikishia ushindi, wachezaji wote waliosafiri wapo salama na wana ari ya ushindani," amesema
Dk Msolla amesema wanaamini matokeo ya mchezo huo yatafahamika baada ya dakika 90 na hayatatokana na utabiri unaofanywa na wale wasioitakia mema Yanga
"Mengi yamezungumzwa kuelekea mchezo huo yakiwa ni kukatishana tamaa, wengine wakidai wachezaji wetu hawawezi kupata matokeo ugenini, hilo halijatutoa mchezoni tuna imani nao na lolote linaweza kutokea ndani ya dakika 90"
Katika mchezo huo Yanga inahitaji angalau ushindi wa mabao 2-0 ili iweze kufuzu hatua ya makundi
Aidha matokeo ya ushindi wa mabao 2-1 kwa Yanga yataupeleka mchezo huo kwenye changamoto ya mikwaju ya penati wakati ushindi wowote wa kuanzia mabao matatu utaipeleka Yanga hatua ya makundi pia