Zahera alia na tiba za wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Nov 2019
Zahera alia na tiba za wachezaji Yanga

Moja ya changamoto zilizoikabili Yanga siku za karibuni ni idadi kubwa ya majeruhi ambayo imepelekea kwa baadhi ya nyota wake kuwa nje kwa muda mrefu

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameeleza kutoridhishwa na huduma walizokuwa wanapewa wachezaji na kitengo cha Utatibu ambacho awali kilikuwa chini ya Dk Edward Bavu

Zahera amesema kwa kiasi kikubwa matunzo duni ya wachezaji wanaoumia yamechangia kutopona kwa haraka na kukaa nje kwa muda mrefu

"Subiri nikwambie kitu, kwanza hamuoni wachezaji wangu wakiumia wanakaa nje muda mrefu? Tatizo wachezaji hawatunzwi," Zahera aliliambia gazeti la Championi

"Mchezaji anaumia nyama za paja lakini matibabu yanachelewa hayaendi kwa wakati kabisa hasa upande wa vipimo"

"Kiukweli hadi leo Paulo Godfrey hajafanyiwa vipimo vya maana, nilimuuliza yule daktari wa mbele (Edward Bavu) kwa nini huyu mtoto haponi na anakaa muda mrefu, shida ni kwamba wachezaji wanatunzwa vibaya"

"Mimi sijui ila nasikiaga kunakuwa na bima na kama wachezaji wapo nayo inasaidiaje, sijui kama wapo nazo maana wachezaji wengi wanalalamika kwa sababu ya kuumia wanakaa muda mrefu kutokana na mambo aliyokuwa anafanya daktari hayakuwa sawa"

Uongozi wa Yanga umefanya mabadiliko kwa kumuajili Daktari mpya Dk Sheki Mgazija kuchukua nafasi ya Dk Edward Bavu

Zahera ameeleza kufurahishwa na utendaji kazi wa Dk Mgazija

"Binafsi ninavyoona kwa daktari huyu mpya katika safari ya Mwanza jinsi anavyofanya kazi yake ni tofauti na yule wa kwanza maana huyu wa sasa amekuwa akiwafuatilia vizuri wachezaji"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’