Zahera kuwakabili 'kivingine' Pyramids Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
3 Nov 2019
Zahera kuwakabili 'kivingine' Pyramids Fc

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera anatarajiwa kukifanyia mabadiliko kikosi chake kitakachoivaa Pyramids Fc leo katika mchezo wa marudiano kusaka tiketi ya kutinga makundi kombe la Shirikisho

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Mwanza na Yanga kufungwa mabao 2-1, Zahera alimtumia Sadney Urikhob kama mshambuliaji pekee huku Papy Tshishimbi akimtumia namba 10

Lakini mabadiliko aliyofanya baadae kwenye kipindi cha pili kwa kuwaingiza Juma Balinya, Patrick Sibomana na Deus Kaseke, yaliiongezea ngvu safu ya ushambuliaji 

Nyota hao wanaweza kuanzishwa kwenye kikosi cha kwanza leo

Nahodha Papy Tshishimbi huenda akarudishwa katika nafasi yake ya kiungo na pengine Balinya kuanzishwa safu ya ushambuliaji pamoja na Sadney

Wawili hao walicheza pamoja mechi dhidi ya Township Rollers iliyopigwa Botswana na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Balinya akifunga bao hilo kupitia mpira wa adhabu

Mabadiliko mengine huenda yakafanyika kwa Sibomana au Kaseke kuchukua nafasi ya Mrisho Ngasa ambaye mchezo wa kwanza haukuwa mzuri sana kwake

Mabadiliko pekee yanayotarajiwa kwenye safu ya ulinzi ni kwa Lamine Moro kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani anayekosa mchezo wa leo akitumikia adhabu ya kadi mbili za njano

Leo Zahera hatakuwa na kikosi pungufu kama ilivyokuwa mchezo wa kwanza hali iliyopelekea kuwajumuisha walinda lango watatu katika kikosi

Yanga imesafiri Misri na kikosi cha wachezaji 20, wachezaji 18 watahitajika kwa ajili ya mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE →