Leo usiku kikosi cha Yanga kitakamilisha maandalizi yake kabla ya kuikabili Pyramids Fc kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho
Yanga iliyowasili Misri Alfajiri ya jana, itafanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa June 30 ambao utatumika katika mchezo huo utakaopigwa kesho Jumapili kuanzia saa tatu usiku
Uwanja huo una uwezo wa kuchukua mashabiki 30,000. Ni moja ya viwanja vilivyotumika kwenye michuano ya Afcon 2019 iliyofanyika mwezi Julai mwaka huu
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wanatarajia kuanza mazoezi yao saa mbili usiku kwa saa za Tanzania
Baada ya mapumziko ya kuondoa uchovu wa safari, leo wachezaji walifanya mazoezi mepesi

Aidha wachezaji walijumuika kufurahi pamoja na kiungo mshambuliaji Issa Bigirimana 'Walcott' ambaye ameadhimisha kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa
