Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa itacheza mchezo wa kirafiki mkoani Tabora Oktoba 18 dhidi ya timu ya daraja la kwanza Rhino Rangers.
Yanga itaelekea mkoani Tabora baada ya mchezo wa ligi, mzunguuko wa sita dhidi Kagera Sugar, mchezo utakaopigwa Oktoba 14.
Yanga itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mpambano wa raundi ya saba ya Ligi Kuu dhidi ya Stand United ya Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga Oktoba 22, mwaka huu.
Rhino inashika nafasi ya sita katika kundi C, nyuma ya vinara wa kundi hilo Alliance ya Mwanza kwa pointi zao 10, wakifuatiwa na Dodoma FC ya Dodoma yenye pointi tisa, wakati JKT Oljoro ina pointi sita, Toto Africans na Transit Camp kila moja pointi nne.
Mara ya mwisho Yanga kucheza Tabora ilikuwa Oktoba 31, mwaka 2015 katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar ambayo wakati huo ilikuwa inautumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

ADVERTISE HERE