Winga Juma Mahadhi anaendele kujiimarisha kwa kufanya mazoezi mepesi baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miezi 15
Hali ya mchezaji huyo imeendelea kuimarika na pengine anaweza kuanza kuonekana dimbani karibuni
Majeraha aliyopata mwezi wa nane mwaka jana, yalikuwa makubwa kiasi kutishia uwezekano wa kuendelea kucheza soka
Hata hivyo baada ya kufanyiwa upasuaji nchini India, nyota huyo ameeleza kuwa yuko katika taratibu za mwisho za matibabu



Mahadhi atakuwa kama ingizo jipya Yanga kwani kwa muda aliokaa nje mambo mengi yamebadilika
Aidha atahitaji kufanya kazi ya ziada ili kurejesha makali yake, ni changamoto ambayo inaweza kuchukua muda
Lakini jambo jema ni kumuona anaweza tena kurejea uwanjani baada ya majeraha yaliyotishia kumaliza maisha yake ya kusakata kabumbu