Balinya kuiongoza Yanga Misri?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Oct 2019
Balinya kuiongoza Yanga Misri?

Wengi wamehoji kwa nini kocha Mwinyi Zahera hampi nafasi mshambuliaji Juma Balinya?

Mara kadhaa Zahera ametoa ufafanuzi kuwa mshambuliaji huyo ameongezeka uzito, ameshuka kiwango na anampa program maalum ili kumrejeshea makali yake

Hata hivyo kwenye mchezo dhidi ya Pyramids Fc ambao Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 jijini Mwanza, kuingia kwa Balinya, Sibomana na Kaseke kuliongeza kasi ya mashambulizi na kuiwezesha Yanga kupata bao kupitia kwa Papy Tshishimbi kwenye dakika ya 88

Kwenye mchezo huo, awali Balinya hakuwa kwenye kikosi cha mechi hiyo lakini jina lake likaongezwa baadae

Zahera amesema mchezo wa Misri, watacheza tofauti na vile walivyocheza Mwanza

Wengi wanasubiri kumuona Balinya akianza na Sadney pale mbele huku Sibomana akichukua nafasi ya Ngasa ambaye anaonekana mechi kubwa zimekuwa changamoto kwake

Baada ya mchezo dhidi ya Pyramids, Balinya alisisitiza kuwa yuko timamu kiafya, yuko tayari kuipigani Yanga ili iweze kufanya vizuri

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’