Suala la madeni bado linaonekana kuitesa Yanga baada ya aliyekuwa kocha wa makipa Juma Pondamali kutishia kwenda kushitaki ngazi za juu kama hatalipwa stahiki zake
Pondamali aliondolewa Yanga mwanzoni mwa msimu na nafasi yake kuchukuliwa na Peter Manyika
Amesema ana madai ya malimbikizo ya mishahara ya miezi saba
"Ninaidai hela nyingi na mara nyingine ukidai unalipwa kidogo kidogo kama laki ama laki mbili, sasa zitaisha lini? Pili inaniuma maana majibu ninayopewa yanauzi sana," amesema
"Nina nyaraka zote muhimu zinazoonyesha kuidai Yanga na kama sitapewa haki yangu, nitakwenda mamlaka nyingine ili kupata msaada wa kulipwa"
Pamoja na jitihada zinazofanyika, bado suala la madeni ni changamoto inayoutesa uongozi wa Yanga
Madeni haya yametokana na malimbizo katika kipindi cha miaka miwili ambayo Yanga ilikuwa na hali mbaya kiuchumi
Beki Andrew Vicent Chikupe mpaka leo amegoma kujiunga na timu akishinikiza alipwe stahili zake
Ni wazi Chikupe huenda akaondoka wakati wa usajili wa dirisha dogo kujiunga na timu nyingine kama ilivyotokea kwa mlinda lango Beno Kakolanya msimu uliopita