Kikosi cha Yanga leo kinafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam kabla ya kutimkia Misri
Yanga itaondoka kesho kuifuata Pyramids Fc tayari kwa mchezo wa marudiano ambao utapigwa Jumapili, Novemba 03 2019
Mabingwa hao wa kihistoria walirejea kutoka Mwanza juzi kwenye mchezo ambao walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1
Baada ya mazoezi makali ya siku mbili, Yanga iko tayari kwa safari ya Misri ambako pia watakuwa na siku chache za maandalizi kabla ya mchezo
ADVERTISE HERE