Mpaka sasa mabosi wa Yanga wameshabaini mapungufu ya kikosi chao na sasa wameamua kuchukua hatua haraka
Achana na suala la Zahera, ni ya maboresho ya timu wakati wa usajili wa dirisha dogo
Wakati fulani tulitaarifu kuhusu kikao kilichofanyika kati ya kiungo Haruna Niyonzima na Abdallah Bin-kleb mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya usajili ya Yanga
Imebainika uongozi wa Yanga tayari umemalizana na Niyonzima na atajiunga na timu usajili wa dirisha dogo ambalo litafunguliwa wiki chache zijazo
Niyonzima alisajiliwa na AS Kigali kwa mkataba wa miezi sita huku akipewa ruhusa ya kuondoka wakati wowote kama atapata timu yenye maslahi zaidi
Kwa lugha rahisi, Niyonzima alijiunga na AS Kigali ili kulinda kiwango chake wakati akisubiri 'dili' zake nyingine
Aidha Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla pia amekamilisha mazungumzo ya kuwasajili beki wa kushoto Erick Rutanga na Michael Sarpong mshambuliaji wa Kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 23 wote wakitokea klabu ya Rayon Sports
Hivi karibuni Dk Msolla alikuwa nchini Rwanda ambako alikutana na Bosi wa klabu ya Rayon
Yanga na Rayon Sports zimeanzisha mpango wa ushirikiano katika kukuza soka la vijana
Nyota hao watatu wanatarajiwa kutua Yanga wakati wa usajili wa dirisha dogo
Hata hivyo Yanga italazimika kuwapiga panga nyota watatu wa kigeni ili kuwasajili wachezaji hao
Inaelezwa tayari uamuzi wa wachezaji watakaopunguzwa umeshafikiwa kinachosubiriwa ni wakati muafaka kukamilisha usajili huo
Yanga imepania kurejesha ubingwa wa ligi kuu ambao wameupoteza kwa wapinzani wao Simba kwa misimu miwili sasa
Aidha baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Pyramids Fc, matumaini ni madogo kwa Yanga kushinda ugenini na kutinga hatua ya makundi
Hivyo upo uwekezano mkubwa kuwa msimu ujao Tanzania itarejea kwenye utaratibu wa kutoa wawakilishi wawili tu kwenye michuao ya CAF
Hivyo msimu huu ni lazima Yanga ishinde taji la ligi kuu au kombe la FA ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao