Wapo wadau wa Yanga wametoa maoni kuwa umefika wakati uongozi wa Yanga ukae chini na kocha Mwinyi Zahera wamuondolee majukumu ya timu ya Taifa
Zipo athari ambazo Yanga imezipata kwa kocha huyo kuwa na majukumu ya timu mbili kwa wakati mmoja
Kabla ya mchezo dhidi ya Pyramids, Zahera alikuwa DR Congo kutimiza majukumu ya timu ya Taifa akarejea nchini wiki moja kabla ya mchezo
Kwa kiasi kikubwa, utaratibu huu unaharibu mtiririko wa mwendelezo wa mazoezi
"Kocha Zahera angepunguziwa majukumu abaki Yanga tu kule Congo mkataba uvunjwe abaki Yanga maana muda mwingi hakai na timu," amesema Elias Simon mdau wa Mwana Jangwani
Lakini pia kocha hana mapumziko, wiki hii yupo Tanzania ijayo Congo na kila mchezo una aproch yake"
"Mfano kocha Etienne Ndayiragije alivyofanyiwa na Azam, hiyo njia itasaidia mwalimu kukaa na timu kwa muda mrefu"
Wengi wanakumbuka wakati wa maandalizi ya msimu, Zahera alikuwa na majukumu ya timu ya Taifa ya DR Congo ambayo ilikuwa ikishiriki michuano ya Afcon 2019
Alirejea nchini wiki mbili kabla ya mchezo wa kwanza dhidi ya Township Rollers
Matatizo ya Yanga kukosa muunganiko yalianza wakati huo, kwani kama angekuwa na timu mapema pengine baadhi ya changamoto leo zisingekuwepo
Hata aliyekuwa kocha Mkuu wa DR Congo Florent Ibenge alijiuzulu nafasi yake baada ya michuano ya Afcon 2019 sasa akibaki na majukumu ya timu ya AS Vita tu
Naamini hata hili la Zahera linaweza kumalizwa na viongozi wa Yanga kulingana na makubaliano ya mkataba
Pengine ni vyema likaangaliwa upya