Pluijm ataweza kufanikiwa tena Yanga?

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
29 Oct 2019
Pluijm ataweza kufanikiwa tena Yanga?

Wakati mjadala wa hatma ya kocha Mwinyi Zahera ukiendelea kushika kasi, kocha wa zamani wa timu hiyo Hans van Pluijm ni miongoni mwa wanaopigiwa chapuo kurithi mikoba ya Zahera huku mwenyewe akibainisha kuwa yuko tayari kurejea Jangwani

Pluijm anakumbuka kwa mafanikio aliyoipa Yanga kwa kutwaa mataji mawili ya ligi kuu msimu wa 2014-15 na 2015-16

Aidha msimu wa mwaka 2016-17 ambao kocha George Lwandamina alitwaa taji la tatu mfululizo, Pluijm alihusika kwenye mzunguuko wa kwanza

Pamoja na kocha huyo kupigiwa chapuo, bado kuna mashaka kama akirejeshwa ataweza kufanikiwa kutokana na hali ya Yanga ya sasa

Kipindi ambacho Pluijm alifanikiwa Yanga, Yusufu Manji alikuwa bado Mwenyekiti na Mfadhili Mkuu

Ni wakati huo ambao wachezaji walilipwa mishahara vizuri na Yanga ilikuwa na uwezo wa kumsajili mchezaji yeyote aliyetakiwa na Pluijm

Nyota kama Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Obrey Chirwa walisajiliwa kwa mapesa mengi

Mfano Chirwa peke yake alitua Yanga kwa dau la Milioni 200!

Lakini kama Pluijm atarejeshwa Yanga leo, atakuta mazingira tofauti

Yanga haina uwezo mkubwa wa kifedha kama ilivyokuwa mwanzo

Aina ya mpira unaofundishwa na Pluijm unahitaji wachezaji wa aina flani ambao kwa sasa Yanga hawapo

Na hata pengine akiwahitaji wachezaji hao, hawawezi kupatikana kwa urahisi kutokana na ufinyu wa bajeti ya usajili

Kwa ufupi, Yanga haina uwezo wa kifedha wa kusajili mchezaji yeyote kama ilivyokuwa wakati wa Manji

Naye hana mbinu mbadala

Wakati baadhi ya mashabiki wakimlaumu Zahera kwa kucheza mpira wa aina moja, hata babu Hans alikuwa akitupiwa lawama hizihizi kabla ya kuondolewa kwenye nafasi yake

Pamoja na kufundisha soka la kuvutia, hakuwa na mbinu mbadala pale timu ilipozidiwa

Ni majuzi tu ametimuliwa Azam Fc

Msimu uliopita Pluijm alitua Azam Fc akitokea Singida United ambayo aliinoa kwa msimu mmoja

Pale Azam Fc alipatiwa kila alichokitaka ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wote aliowataka

Aliwachukua Donald Ngoma na Obrey Chirwa kutoka Yanga pamoja na kusajili wachezaji wengine

Lakini baada ya miezi saba Azam Fc ilimfungashia virago pamoja na Juma Mwambusi aliyekuwa kocha Msaidizi

Hapa jambo la kujiuliza Pluijm alishindwa kufanikiwa Azam Fc ambayo ina kila kitu ataweza kufanikiwa na Yanga hii ya sasa ambayo ni ya kuunga-unga?

Soka la Tanzania linabadilika kwa kasi sana, mbinu ambazo zilikupa mafanikio jana zinaweza zisikupe mafanikio leo

Ushauri kwa uongozi wa Yanga kama wanaona kuna ulazima kufanya mabadiliko benchi la ufundi basi ni bora wakaangalia makocha wa hapahapa nchini wawape timu mpaka mwishoni mwa msimu

La sivyo ni bora kuendelea na Zahera ambaye kikosi hiki amekiunda yeye, mpaka asasa amefahamu udhaifu ulipo anachohitaji ni muda ili kuondoa mapungufu yaliyopo

Lakini pia Yanga iliunda Kamati ya Ufundi ambayo ina watu kama kocha Charles Mkwasa (Katibu), Ally Mayay, kocha Ken Mwaisabula, Sunday Manara na wengine ambao ni wabobezi wa soka

Kamati hii iliundwa mahsusi kulisaidia benchi la ufundi

Nadhani kama wakiifanya kazi yao vizuri, kwa kushirikiana na kocha Zahera, wanaweza kuondoa baadhi ya mapungufu ambayo wengi wanaamini yanaikwaza Yanga kufanya vizuri

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’