Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mchezo wa marudiano wanaokwenda kucheza Misri dhidi ya Pyramids Fc utakuwa tofauti na ule waliocheza jijini Mwanza
Mcongomani huyo ambaye siku ya jana tetesi zilishamiri kuwa anaweza kusitishiwa mkataba wake, amesema mchezo wa Misri watacheza kwa kufunguka
"Mbinu tutakazotumia mchezo wa ugenini ni tofauti na vile tulivyocheza hapa nyumbani. Tunahitaji ushindi hivyo tutaiandaa timu yetu kuweza kutimiza lengo hilo"
"Tunao wachezaji wazuri ambao wanaweza kutupatia matokeo Misri hivyo lolote linaweza kutokea," amesema
Hahofii kutimuliwa Yanga
Katika hatua nyingine Zahera amesema suala la yeye kuendelea kuinoa Yanga au la liko mikononi mwa viongozi
Amesema hana mpango wa kujiuzulu, lakini viongozi wa Yanga wakiamua kusitisha mkataba wake, hatakuwa na tatizo

"Makocha wanaajiliwa ili wafukuzwe hivyo mimi sina wasiwasi kama hilo litatokea. Nikiondoka Yanga siwezi kukosa kazi, timu nyingi zinanitaka," alisema kocha huyo ambaye pia anaifundisha timu ya Taifa ya DR Congo
"Lakini kwa sasa naendelea na majukumu yangu Yanga kwani mkataba wangu bado upo mpaka mwishoni mwa msimu"