Yanga yajipanga 'kupindua meza' Misri

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Oct 2019
Yanga yajipanga 'kupindua meza' Misri

Uongozi wa klabu ya Yanga umewaomba radhi mashabiki wake baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa kombe la Shirikisho kwa kufungwa mabao 2-1 na Pyramids Fc juzi

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema wanafahamu matokeo hayo yamewaumiza mashabiki na wanachama wao ambao walikuwa na matumaini makubwa ya kushinda katika mchezo huo uliopigwa jijini Mwanza

Amesema timu inajiandaa kwenda kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Novemba 03 nchini Misri akikiri kuwa watahitaji kufanya kazi ya ziada kuweza kupata matokeo

Ten amesema Yanga itaondoka keshokutwa Alhamisi, Oktoba 31 kuelekea Misri tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa Jumapili

Nae Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela amesema pamoja na kupoteza mchezo wa kwanza, hawajakata tamaa, watakwenda Misri wakiwa na lengo la kusaka ushindi

"Hata siku moja hatuwezi kukata tamaa, tunakwenda Misri tukiwa na lengo la ushindi. Tumewaona Pyramids, tunaweza kuwafunga kwao," amesema

Katika michezo yote waliyocheza msimu huu kwenye michuano ya CAF, Yanga haikushinda nyumbani lakini timu imeonekana kuimarika zaidi inapocheza ugenini

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’