Mkurugenzi wa Udhibiti na Uendeshaji wa SportPesa ambaye pia ni Mwanachama wa klabu ya Yanga, Tarimba Abbas amesema kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera hapaswi kulaumiwa juu cha kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Pyramids ya Misri walichopata jana.
Tarimba amesema kipigo cha jana katika uwanja wa CCM Kirumba kimetokana na uzembe wa moja kwa moja kutoka kwa wachezaji na sio kosa la kocha Zahera.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa bao la pili walilofungwa lilitokana na Mrisho Ngasa kuacha kukaba akidhani mpira ulikuwa umetoka wakati mwamuzi hakupiga filimbi huku lile la kwanza likitokana na uzembe wa Papy Tshishimbi
"Sijaona kosa la kocha Zahera, wachezaji wenyewe walifanya makosa ya kizembe ambayo wenzetu waliyatumia na kupata matokeo ugenini," amesema
Aidha Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga amesema Pyramids Fc sio timu ngumu, wanafungika kama Yanga watajipanga vizuri wanaweza kupata ushindi ugenini