Lwandamina vs Pluijm michezo mitano ya kwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Oct 2017
Lwandamina vs Pluijm michezo mitano ya kwanza
SINGIDA UNITED

Singida United inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga Hans van Pluijm ni moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri msimu huu.

Mpaka kukamilika kwa mzunguuko wa tano Singida United inashika nafasi ya nne baada ya kushinda michezo mitatu, kutoka sare mmoja na kufungwa mmoja. Ina alama 10

Matokeo yake yako hivyi;

Mwadui 2-1 Singida United
Singida United 2-1 Mbao FC
Stand United 0-1 Singida United
Singida United 1-0 Kagera Sugar
Singida United 1-1 Azam FC

Imefunga mabao sita na imefungwa mabao manne.

YANGA

Yanga inanolewa na kocha George Lwandamina, aliyechukua mikoba ya Pluijm ambaye awali alipewa cheo cha Ukurugenzi wa Ufundi kabla Yanga haijafuta cheo hicho na yeye kutimkia Singida United.

Yanga inashika nafasi ya sita, ikiwa na alama tisa. msimu huu imeshinda michezo miwili na kutoka sare michezo mitatu.

Matokeo yake;

Yanga 1-1 Lipuli
Njombe 0-1 Yanga
Majimaji 1-1 Yanga
Yanga 1-0 Ndanda
Yanga 0-0 Mtibwa

Imefunga mabao manne, imefungwa mawili na ina alama tisa ikiwa inashika nafasi ya sita.

Ukitathmini takwimu za makocha hao utaona tofauti baina yao ni ndogo. Timu zao zinatofautiana kwa alama moja tu Pluijm akiwa mbele.

Aidha licha ya kufunga mabao manne, ukuta wa Yanga umeruhusu mabao mawili tu huku Singida United ikiwa imefunga mabao sita na kufungwa mabao manne. Timu zote zina tofauti ya uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa sawa (+2).

Tumeweka takwimu hizi makusudi kuwasaidia wale wanaoamini kama Yanga ingekuwa inanolewa na Pluijm pengine ingekuwa katika nafasi nzuri zaidi kuliko ilivyo sasa.

Takwimu hizo zinakuonyesha kuwa tatizo pekee la Yanga ni kwenye safu ya ushambuliaji (imefunga mabao machache) lakini imeimarika sana kwenye safu yake ya ulinzi.

Hata ukichukua takwimu za msimu uliopita za kocha Pluijm kwenye michezo yake mitano ya kwanza wakati akiwa Yanga na takwimu za Lwandamina katika michezo yake mitano ya kwanza msimu huu utaona tofauti ya alama baina ya makocha hao ni moja.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’