Wakati Yanga ikihitaji matokeo ya ushindi kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Pyramids Fc nchini Misri, mabingwa hao wa kihistoria watamkosa beki wao kisiki Kevin Yondani ambaye jana hakumaliza mchezo baada ya kupewa kadi nyekundu
Yondani alitolewa kwenye dakika za majeruhi baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano
Hata hivyo beki Lamine Moro atarejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kadi nyekundu
Lamine naye alilimwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa pili dhidi ya Zesco United
Aidha uwepo wa beki Ali Ali bado unaongeza matumaini safu ya ulinzi ya Yanga kwenye mchezo huo utakaopigwa Jumamosi nchini Misri
Bila shaka, Ali atacheza na Lamine safu ya ulinzi wa kati
Yanga inahitaji ushindi wa kuanzia mabao mawili nchini Misri ili kuwa na nafasi ya kutinga hatua ya makundi
Β