Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ni wachezaji watatu tu ambao hawataweza kucheza mechi ya kesho dhidi ya Pyramids Fc kutokana na kuwa majeruhi
Nyota hao ni Maybin Kalengo, Raphael Daudi na Paulo Godfrey ambaye bado hayuko fit baada ya kurejea kikosini hivi karibuni
Aidha kuhusu hatma ya mshambuliaji Sadney Urikhob, Zahera amesema mshambuliaji huyo amerejea kikosini baada ya kupata mapumziko ya siku tatu
Sadney alipata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc
ADVERTISE HERE