Wachezaji wa Pyramids Fc waliwasili jana jioni jijini Mwanza kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Timu hiyo imetua Mwanza kwa usafiri wa ndege binafsi
Pyramids iliwatanguliza baadhi ya maafisa wake ambao wamekuwepo Mwanza kwa takribani siku tatu
Timu hiyo kuja nchini na ndege binafsi sio jambo la kushangaza, kwani ni timu yenye 'ukwasi'
Lakini watakuwa na kazi dimba la CCM Kirumba dhidi ya Yanga ambayo imejipanga kwelikweli
ADVERTISE HERE