Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka keshokutwa Alhamisi kuelekea mkoani Kagera kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Oktoba 14 katika dimba la Kaitaba.
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea Shinyanga ambako itachuana na Stand United.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema Yanga itaondoka jijini Dar es salaam na wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza isipokuwa Donald Ngoma ambaye bado ni majeruhi
Ten amesema ukimuondoa Ngoma, wachezaji wengine wapo sawa jambo ambalo linawapa matumaini ya kutimiza kile ambacho wamekikusudia kukifanya kwenye mechi hizo.
Ten amesema wanakwenda kanda ya ziwa kuchukua alama zote sita kwa kuibuka na ushindi katika michezo dhidi ya Kagera Sugar na Stand United.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea mazoezini leo baada ya mapumziko ya siku moja.

ADVERTISE HERE