Mshambuliaji wa Yanga Sadney Urikhob amepata majeraha ya kifundo cha mguu yaliyomfanya ashindwe kufanya mazoezi leo
Sadney alipata majeraha hayo kwenye mchezo dhidi ya Mbao Fc ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo alilifunga yeye
Daktari wa Yanga Dk Sheki Mgazija amesema majeraha hayo sio makubwa ambapo matibabu yake mpaka kupona kabisa yanaweza kuchukua siku tatu
Baada ya mshambuliaji David Molinga kukosa kibali, Sadney ndiye anayetizamwa kuibeba Yanga katika mchezo dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa Jumapili
Kama hataweza kupona kwa wakati kocha Mwinyi Zahera atalazimika kumtumia Mganda Juma Balinya ambaye siku za karibuni amekuwa hapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Jana Balinya alifunga moja ya mabao ya Yanga kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Fc ukiwa ni mchezo wa kirafiki