Kamati ya uhamasishaji ya Yanga kwa kushirikiana na wadau wengine, wameweka nguvu katika kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc siku ya Jumapili
Pamoja na kupunguzwa kwa bei ya viingilio, Kamati hiyo inayoongozwa na Rogers Gumbo kama Mwenyekiti itakuwa na jukumu la kuwahamasisha mashabiki waujaze uwanja wa CCM Kirumba ambao unachukua mashabiki wanaokadiriwa kufika 40,000
Viingilio vya mchezo huo vimepunguzwa ambapo sasa kiingilio cha juu kabisa Royal ni TSh 50,000/- wakati VIP ni Tsh 20,000/-
Mzunguuko ambao ndio huchukua mashabiki wengi, kiingilio chake ni Tsh 7,000/-
Pamoja na kuhitaji sapoti ya mashabiki, uongozi wa Yanga umejipanga kuhakikisha ushindi unapatikana Jumapili
Kumekuwa na vikao vinavyofanyika vikiwahusisha viongozi, wachezaji na wadau wa Yanga jijini Mwanza ili kuhakikisha Pyramids wanafungwa
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kikosi kiko vizuri, wachezaji wanaendelea na maandalizi viongozi wakihakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kambi ya timu hiyo