Mayanga aomba radhi mashabiki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
9 Oct 2017
Mayanga aomba radhi mashabiki
Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Salum Mayanga amewaomba radhi mashabiki wa soka nchini kwa matokeo yasiyo mazuri kwenye mechi dhidi ya Malawi iliyopigwa Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Mayanga amesema anayafanyia kazi mapungufu na kuahidi kuwa timu itafanya vizuri katika michezo inayokuja.

“Naomba mashabiki watusamehe kwa matokeo ya mchezo uliopita, nimeyaona mapungufu ya timu na nitayafanyia kazi ili tuweze kushinda kwenye mechi zijazo”.

Aidha Mayanga ameeleza nia yake ya kupata michezo miwili ya kirafiki ili kujiweka vyema na mchezo wake wa kuwania kufuzu AFCON 2019 dhidi ya Uganda Machi 2018.

Taifa Stars imekuwa haina mwendelezo wa matokeo mazuri ambapo ikumbukwe kuwa iliifunga Malawi kwenye michuano ya COSAFA lakini imeshindwa kufanya hivyo kwenye uwanja wa nyumbani.

Tanzania ipo Kundi L na timu za Uganda, Cape Verde na Lesotho kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019 nchini Cameroon.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
46m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →