Jana kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alimaliza adhabu ya kukosa mechi tatu alipokaa jukwaani wakati Yanga ikiikabili Mbao Fc kwenye mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba
Pamoja na kutokaa kwenye benchi katika mechi hizo, Yanga imekusanya alama saba kati ya tisa
Mechi ya kwanza aliyokosa ilikuwa dhidi ya Polisi Tanzania ambapo Yanga ililazimishwa sare ya mabao 3-3
Akakosa mechi dhidi ya Coastal Union ambayo Yanga ilishinda 1-0 na jana pia mabingwa hao wa kihistoria wakipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao
Tangu afungiwe Zahera pamoja na kupigwa faini ya Tsh Laki Tano baada ya kuvaa 'pensi', hakuna kocha mwingine aliyekumbana na adhabu ya TFF
Wadau wa Yanga wanasubiri kuona nini kitajiri kati yake na TFF baada ya kocha huyo kurejea kwenye benchi la ufundi
Maana kumekuwa na dhana kuwa ni kama TFF imepania kumnyima uhuru wa kuongea kocha huyo tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita