Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi Jumapili Oktoba 27 kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Mbao Fc jana ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0, Tshishimbi amesema mchezo wa Jumapili watafanya zaidi ya kile walichofanya kwenye mchezo huo
"Mashabiki waje kwa wingi kutuunga mkono Jumapili. Leo tumetengeneza nafasi nyingi lakini tumeitumia moja. Tunawaahidi Jumapili tutafunga mabao mengi," amesema
Katika mchezo wa jana, kikosi cha Yanga kilionenaka kuwa imara dhidi ya wapinzani wao, kikitawala mchezo huo
Bao pekee la ushindi lilifungwa na Sadney Urikhob ambaye kama angekuwa makini angeweza kufunga hat-trik
Aidha mlinda lango wa Mbao Fc alifanikiwa kuokoa mipira mitatu ya adhabu iliyopigwa kiufundi na David Molinga huku Tshishimbi akikosa bao baada ya mpira wake wa kichwa kugonga mwamba
Mshambuliaji Juma Balinya aliyeingia dakika ya 76 kuchukua nafasi ya Molinga nae akakosa bao wakati mchezo huo ukielekea ukingoni
Kwa ujumla, kikosi cha Yanga kilionyesha utayari wa kuwakabili Pyramids Fc Jumapili