Kocha msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema benchi la ufundi linafanyia kazi tatizo la umaliziaji linaloikabili safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.
Akizungumza baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya KMC, Nsajigwa amesema Yanga ilicheza vizuri katika mchezo huo lakini bado mapungufu katika safu ya ushambuliaji yameendelea kuinyima Yanga ushindi.
"Kuna tatizo kwenye safu ya ushambuliaji, mabao yanakataa, timu haifungi ni jambo linalotuumiza na tunaendelea kuhangaika nalo ili kuhakikisha tunarejea katika ubora wetu," amesema Nsajigwa
"Wachezaji wengi wanaocheza eneo hilo ni wagonjwa na wengine hawako fiti pia ukiangalia hata katika mchezo huo tumetumie baadhi ya wachezaji ambao hawachezi mara kwa mara."
Yanga inajiandaa na mzunguuko wa sita ligi kuu ya Vodacom ambapo Oktoba 14 itakuwa ugenini dimba la Kaitaba kuumana na Kagera Sugar.
Katika mchezo huo huenda ikawakosa washambuliaji wake Donald Ngoma na Obrey Chirwa ambao walipata majaraha katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Amissi Tambwe anaweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kupona majeraha ya goti yaliyomuweka nje kwa miezi miwili.

ADVERTISE HERE