Kikosi cha Yanga jioni ya leo kimefanya mazoezi kwenye uwanja wa CCM Kirumba yakiwa ni maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc
Mchezo huo utapigwa kesho Jumanne katika uwanja huo
Kwenye mazoezi hayo, wachezaji wameonyesha ari na utayari wa kuwakabili Mbao Fc hapo kesho
Mkufunzi wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema anatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa Mbao lakini wamejiandaa kushinda
"Mchezo huu ni muhimu kwetu kushinda ili kuweka juu morali ya wachezaji kuelekea mchezo dhidi ya Pyramids Fc," amesema
"Tunafahamu jinsi Mbao Fc wanavyocheza wanapokutana na sisi, tumejiandaa vizuri kukabiliana nao"
ADVERTISE HERE