Mlinda lango Metacha Mnata na kiungo Abdulaziz Makame waliokuwa timu ya Taifa, wameripoti kambi ya kikosi cha Yanga jijini Mwanza kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc ambao utapigwa kesho Jumanne kwenye uwanja wa CCM Kirumba na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa Oktoba 27
Aidha kiungo mshambuliaji Issa Bigiramana ambaye alikuwa majeruhi, nae amewasili jijini Mwanza kuendelea na maandalizi hayo baada ya kupona
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli, Mohammed Issa 'Banka' na Cleofas Sospeter wao wanaendelea na matibabu ya majeraha yanayowasumbua
Kikosi kamili kilichoweka kambi Mwanza
1. Metacha Mnata
2. Farouk Shikhalo
3. Ramadhani Kabwili
4. Paulo Godfrey
5. Juma Abdul
6. Ally Mtoni
7. Muharami Mohammed
8. Lamine Moro
9. Ally Ally
10. Mustafa Suleyman
11. Kelvin Yondani
12. Abdulaziz Makame
13. Papy Tshishimbi
14. Feisal Salum
15. Raphael Daudi
16. Said Juma
17. Jaffar Mohammed
18. Gustafa Simon
19. Issa Bigirimana
20. Deus Kaseke
21. Mrisho Ngasa
22. Patrick Sibomana
23. Sadney Urikhob
24. Juma Balinya
25. David Molinga
26. Maybin Kalengo
27. Mapinduzi Balama