Uongozi wa klabu ya Yanga umetimiza ahadi yake ya kupunguza bei ya viingilio vya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa Jumapili Oktoba 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema baada ya kupokea malalamiko, mapendekezo, maoni na ushauri kutoka kwa wadau, wamepunguza bei hizo za viingilio
Hii hapa bei mpya za viingilio;
Royal - Tsh 50,000/-
VIP - Tsh 20,000/-
Mzunguuko - Tsh 7,000/-
Aidha Mwakalebela amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Oktoba 27 kuiunga mkono timu yao ili kuhakikisha wanashinda mchezo wa kwanza dhidi ya Pyramids Fc
Amewataka wadau wote kukata tiketi halali ili pamoja na kupata burudani, waweze kuichangia timu yao kupitia viingilio hivyo
"Baada ya makato yote, Yanga tutapata asilimia 42 ya mapato yote yatakayopatikana. Hivyo tunawaomba mashabiki na wadau wote kukata tiketi halali na kuingia uwanjani kwa utaratibu rasmi uliowekwa."