Bodi ya ligi yakana kumuandaa Magori kumrithi Wambura

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Oct 2019
Bodi ya ligi yakana kumuandaa Magori kumrithi Wambura

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPBL), imekanusha madai ya kumuandaa aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori kurithi nafasi ya Boniface Wambura kuwa Mtendaji Mkuu wa bodi hiyo.

Magori amekuwa akihusishwa kuandaliwa kuchukua nafasi ya Wambura tetesi zikishika kasi baada ya TFF kumbadilishia majukumu Wambura

Mwenyekiti wa bodi hiyo, Steven Mgutto amesema ajira ya Mtendaji wa Bodi ya Ligi itatangazwa na wagombea watapaswa kutuma maombi

"Ndani ya siku mbili hizi tunatarajia kutoa tangazo la nafasi za kazi kwa ajili ya kutafuta mrithi wa Wambura ambapo kuna vigezo mbalimbali vinatakiwa kuwepo kwa mgombea anayehitaji kuwania nafasi hiyo, lengo ni kuwa na kiongozi bora," amesema

"Kuhusu suala la Magori nimekuwa nikisikia kutoka kwa watu mbalimbali kuwa ndiye aliyepangwa kurithi nafasi ya Wambura lakini si kweli, ila iwapo atahitaji kuwania nafasi hiyo ni vyema akawasilisha wasifu wake kama ilivyo kwa wadau wengine watakaojitokeza kuomba nafasi hiyo kulingana na vigezo vitakavyotolewa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’