Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wamejiandaa kikamilifu kuelekea mchezo dhidi ya Mbao Fc ligi kuu ya Vodacom ambao utapigwa Jumanne, Oktoba 22
Akizungumza baada ya kuwasili jijini Mwanza mapema leo, Zahera amesema kikosi chake kimefanya maandalizi ya kutosha
"Tumejipanga kucheza kufuatana na wapinzani wetu tutakaokabiliana nao, tupo tayari kucheza na Mbao," alisema Zahera
"Tumekuja na wachezaji wetu wote waliotimamu ambapo wale wawili (Abdulaziz Makame na Metacha) waliopo Taifa Stars watawasili kesho hapa Mwanza, leo tutaanza mazoezi tayari kuelekea michezo ijayo"
ADVERTISE HERE