Kwa hali ilivyo ni dhahiri Yanga haiwezi kukwepa kusajili mshambuliaji atakayeweza kuongeza nguvu ya ushambulizi katika kikosi cha kocha George Lwandamina.
Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Donald Ngoma walitarajiwa kuwa washambulizi viongozi sambamba na Ibrahim Ajib.
Lakini ni Ajib pekee aliye katika kiwango bora huku Tambwe akiwa bado hajacheza mchezo wowote wa ligi msimu huu akisumbuliwa na majeruhi.
Ngoma nae ameingia katika orodha ya majeruhi sawa na Chirwa.
Tambwe na Chirwa kwa sasa hawapo katika kikosi cha Yanga walipewa ruhusa maalumu kurudi makwao kushughulikia matatizo ya kifamilia.
Wanatarajiwa kurejea kabla ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 14.
Yanga inakabiliwa na changamoto ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne pamoja na michuano ya klabu bingwa mwakani.
Inahitaji kuimarsisha kikosi chake ili kuweza kufanya vizuri katika michuano hiyo.

ADVERTISE HERE