Suala la Molinga, Mustafa bado utata

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Oct 2019
Suala la Molinga, Mustafa bado utata

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema mshambuliaji David Molinga na beki Mustafa Suleyman wataanza kuitumikia timu hiyo kuanzia hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho iwapo watafanikiwa kuitoa Pyramids Fc

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwakalebela amesema kulingana na kanuni za CAF za michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho haziwaruhusu kucheza hatua ya mtoano

"Napenda nitoe ufafanuzi kuhusu wachezaji wawili ambao watu wamekuwa wakiuliza kama wataweza kucheza mechi dhidi ya Pyramids Oktoba 27"

"Ni suala la kikanuni kwamba wachezaji Molinga na Mustafa wataruhusiwa kuitumikia Yanga kama tutatinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa au kombe la Shirikisho"

"Hivyo wachezaji hao tutaendelea kuwatumia kwenye ligi na kama tutatinga makundi wataweza kucheza," amesema

Taarifa hiyo inakinzana na ile iliyotolewa wiki iliyopita na Afisa Habari Hassan Bumbuli ambaye alisema Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) lilikuwa limewahakikishia kuwa wachezaji hao wataruhusiwa kucheza na kinachosubiriwa ni kuwasili kwa vibali vyao

Ni wazi baada ya kufuatilia huko CAF, Yanga imejiridhisha haitaweza kuwatumia wachezaji hao kwa ajili ya mchezo dhidi ya Pyramids FC

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’